Kesi hiyo inatokana na mashtaka mawili yaliyofikishwa mbele ya seneti kuhusiana na kadhia ya Ukraine ambapo inadaiwa Rais Trump alitumia vibaya madaraka yake kwa kuzuia msaada wa kijeshi kwenda Ukraine.
Baraza la Seneti : Matukio muhimu ya kesi inayoendelea dhidi ya Rais Donald Trump
Baraza la Seneti la Bunge la Marekani laanza kusikiliza hoja za awali juu ya kesi inayotaka kumuondoa Rais Donald Trump madarakani, Jumatano, Januari 22, 2020.

5
Kiongozi wa waliowengi katika Baraza la Seneti Mitch Mc Connell, kulia, akiwa na Katibu wa waliowengi Laura Dove, kushoto, akirejea katika ukumbi wa Bunge mjini Washington, Jumanne usiku, Januari 21, 2020.(AP Photo/J. Scott Applewhite)

6
Jaji Robert Johnson akiongea wakati wa kuanza kwa kesi ya kumuondoa madarakani Rais Donald Trump.

7
Usiku wa Jumanne, Januari 21, 2020, ambapo kesi dhidi ya Rais Donald Trump iliendelea kusikilizwa hadi usiku wa manane.

8
Maseneta wakipiga kura kuwasilisha marekebisho yaliyoletwa na Kiongozi wa Wademokrat waliowachache katika Baraza la Seneti Chuck Schumer, katika Ukumbi wa Bunge la Marekani, Jumatano, Jan. 22, 2020. (Senate Television via AP)