Balozi za Marekani katika nchi kadhaa zilikabiliwa na waandamanaji, walioghadhibishwa na kifo cha George Floyd kilichotokea Mei 25. Floyd alifariki baada ya polisi mzungu kuweka goti lake kwenye shingo lake kwa takriban dakika 9.
Dunia yalaani kifo cha Mmarekani mweusi akishikiliwa na polisi
Maandamano yamefanyika katika miji mbalimbali duniani Jumamosi, ikiwa ni mshikamano wa namna fulani na waandamanaji wa Marekani kufuatia kifo cha Mmarekani mweusi wakati akiwa mikononi mwa polisi mapema wiki hii.

13
Waandamanaji wakipambana na polisi wakati wa maandamano ya kulaani kifo cha George Floyd, Jumamosi, Mei 30, 2020 karibu na White House mjini Washington.

14
Waandamanaji wakilaani kifo cha George Floyd, Jumamosi, Mei 30, 2020 karibu na White House mjini Washington.

15
Polisi wakimkaribia Mwandamanaji baada ya kutangazwa amri ya kutotoka usiku, Ijumaa Mei 30, 2020, huko Minneapolis. (AP Photo/John Minchillo)