Hatua hiyo inafuatia kujiuzulu Jumamosi kwa Mkuu wa Polisi wa mji wa Atlanta Erika Shields, baada ya Rayshard Brooks, umri miaka 27, kuuawa Ijumaa, na kusababisha wimbi jipya la maaandamano mjini Altanta baada ya kuwepo maandamano makubwa yakulaani kifo cha George Floyd akiwa chini ya ulinzi wa polisi huko Minneapolis yaliyokuwa yamepungua kasi.
Ghasia, maandamano yazuka Atlanta baada ya kifo cha mtu mweusi
Afisa wa polisi mjini Atlanta afukuzwa kazi baada ya kupiga risasi iliyosababisha kifo cha mtu mweusi na afisa mwengine amepangiwa kazi nyingine za kiutawala, idara ya polisi imetangaza mapema Jumapili

9
Waandamanaji wakusanyika katika mtaa wa University ulioko karibu na Mgahawa wa Wendy, Jumamosi, Juni 13, 2020 mjini Atlanta. Utawala wa Georgia ulisema Jumamosi mtu mmoja alipigwa risasi na kuuawa katika purukushani iliyotokea kati yake na polisi wa Atlanta usiku mwingi nje ya mgahawa wa Wendy. (AP Photo/Brynn Anderson)