Watu walioshuhudia tukio hilo wanasema vikosi vya usalama vilifyatua mabomu ya machozi na maguruneti ndani ya msikiti, wakati wanaofanya ibada walirusha mawe na vitu vingine kuwalenga askari hao. Shirika la Hilal Ahmar limesema zaidi wa Wapalestina 300 wamejeruhiwa, kati yao 228 walipelekwa hospitali ya karibu. Darzeni ya Wapalestina walijeruhiwa.
Mapambano yazuka tena Jerusalem karibu na msikiti wa al-Aqsa
Mapambano mapya yamezuka Jumatatu kati ya vikosi vya usalama vya Israeli na Wapalestina waliokuwa wanafanya ibada karibu na msikiti wa al-Aqsa mjini Jerusalem Jumatatu.

6
Mwanamke wa Kipalestina akiwa karibu na vikosi vya usalama vya Israeli wakati wa machafuko kati ya Waisraeli na Wapalestina huku Israeli ikiadhimisha Siku ya Jerusalem, katika eneo la Damascus Gate nje ya mji wa Old City, Jerusalem, Mei 10, 2021. REUTERS/Ronen Zvulun

7
Wapalestina wakijihami baada ya vikosi vya usalama vya Israeli kutupa maguruneti, Mei 9, 2021. (Foto: Ronen Zvulun/Reuters)

8
Wapalestina wakikabiliana na vikosi vya usalama vya Israel katika ghasia zinazo endelea Jerusalem.