Wamarekani wanapo omboleza vifo vya wanafunzi 19 wa shule ya msingi ya Robb mjini Uvalde, Texas, wabunge mjini Washington wanaendelea kujadili kwa hamasa suala la kupitisha sheria za kudhibiti umiliki wa bunduki.
Shambulizi katika shule ya msingi Uvalde, Texas
Kijana mwenye umri wa miaka 18 alishambulia kwa bunduki shule ya msingi ya Robb, mjini Uvalde, Texas na kusababisha vifo vya watoto 19 na walimu wawili.

9
Watoto wanabeba maua nje ya kituo cha Ssgt. Willie de Leon Civic, ambako wanafunzi walipelekwa baada ya shambulio kwenye shule ya Robb Elementary Uvalde, Texas, May 24, 2022.

10
Rais Joe Biden, akiwa na huzuni na hasira akilihutubia taifa kufuatia mauwaji kwenye shule ya msingi mjini Uvalde, Texas, muda mfupi baada ya kurudi kutoka ziara ya Japan. May 24, 2022.

11
Watoto wakingia kwenye basi ya shule wakilindwa wa maafisawa usalama baada ya shambulio katika shule yao ya Robb Elementary mjini Uvalde, Texas, May 24, 2022.

12
Bendera ya Marekani yapepea nusu mlingoti juu ya White House kuomboleza mauwaji ya shule ya msingi ya Robb Elementary mjini Uvalde, Texas, May 24, 2022.