Rais Biden aliweka shada la maua nje ya jengo ambalo ndege nambari 93 ilianguka huku mvua ikinyesha. Akiwahutubia walohudhuria sherehe hizo, alitaja jinsi wamarekani walivyoungana kujibu mashambulio hayo na kuapa kwamba “kamwe hawatoacha” kuendelea kupigana dhidi ya vitisho vya ugaidi.
Wamarekani waadhimisha miaka 21 tangu mashambulio ya kigaidi ya Septemba 11, 2001
Rais Joe Biden aliongoza ibada kwenye jengo la Pentagon, huku Makamu Rais Kamala Harris akiungana na waombolezi mjini New York na mke wa rais Jill, aliongoza ibada Pennsylvania ili kuwakumbuka watu elfu 3 walofariki kwenye maeneo hayo.

5
Rais Joe Biden akiweka shada la maua wakati wa kuadhimisha miaka 21 ya mashambulio ya Septembe 11 nje ya jengo la Pentagon.

6
Watu walokusanyika kwenye mtaa wa Cedar wakati wa sherehe za kuadhimisha miaka 21 tangu mashambulio ya Septemba 11, 2001.

7
Watu wakitoa heshima zao kwenye uwanja wa makumbuko ya mashambulio ya Septemba 11 mjini New York.

8
Familia za waathiriwa na wageni wanaohudhuria sherehe za miaka 21 tangu mashambulio ya Septemba 11 nje ya jengo la Pentagon.