Akiwa katika nchi hizo mbili Papa Francis alitoa ujumbe muhimu wa kutaka mapigano na ghasia kukomeshwa mara moja, na kudumishwa kwa amani katika nchi hizo mbili za Afrika ya Kati.
Papa Francis akamilisha ziara yake ya Sudan Kusini na DRC
Papa Francis amekamilisha ziara yake ya siku 6 nchini Sudan Kusini na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, kwa Misa Takatifu kwenye uwanja wa makumbusho wa John Garang, mjini Juba, siku ya Jumapili.

5
Wananchi wa Sudan Kusini wasikiliza hotuba ya Papa Francis wakati wa Misa Takatifu mjini Juba.

6
Papa Francis akiwapungia mkono waumini alipokua anazunguka ndani ya gari lake kwenye uwanja wa John Garan mjini Juba.

7
Makasisi na Watawa wahudhuria Misa Takatifu inayoongozwa na Papa Francis.

8
Waumini wanaimba Kwaya wakati Papa Francis akiongoza Misa mjini Juba.