Michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika AFCON 2019
AFCON 2019 MISRI : Ratiba ya Raundi ya 16

Raundi ya 16 inaanza leo mjini Cairo, Misri.
Usikose kufuatilia mechi hizi kupitia mitandao yetu yote na vipindi vyetu vya radio na televisheni...
See all News Updates of the Day
Mambo yanavyoendelea Cameroon kwenye AFCON
Mambo yalivyo Cameroon wakati AFCON ikiendelea
Algeria yashinda Kombe la AFCON 2019 kwa kuichapa Senegal 1-0

Baghdad Bounedjah katika dakika za mwanzo aliipatia timu ya Algeria bao la ushindi katika Michuano ya Fainali ya Michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika, AFCON, 2019, Kombe la AFCON, Ijumaa, ambapo ilishiriki kwa mara ya kwanza baada ya kipindi cha miaka 29.
Algeria walipata ushindi wa bao moja kwa sifuri dhidi ya timu ya Senegal katika michuano ya finali hiyo iliyofanyika mjini Cairo.
Bounedjah alifanikisha mwanzo wa ndoto ya Algeria, katika dakika ya pili, golikipa wa Senegal Alfred Gomis aliyepitwa na mpira uliotinga katika nyavu ya goli lake.
Goli hilo lilitokana na mpira uliopigwa na Baghdad kumgonga mchezaji wa Senegal Salif Sane na kumpita nduki mlinzi wa lango la Senegal, Alfred Gomis.
Na hapo ndipo ilikuwa ni uthibitisho wa kutosha kwa mabingwa wa mwaka 1990 kuwa watachukuwa kombe katika mchezo wa ugenini kwa mara ya kwanza.
Rais wa muda wa Algeria Abdelkader Bensaleh naye aliwasili dimbani kushuhudia mchuano huo, jambo ambalo liliwapo moyo wachezaji wa timu yake.
Senegal, timu ambayo haijawahi kutwaa ushindi katika michuano ya AFCON walipewa penalti baada ya mchezaji wa Algeria kuunawa mpira lakini refa alibadilisha uamuzi huo.
Wachambuzi wanasema Senegal wakishiriki kwa mara ya pili katika fainali tangu 2002, walikuwa wakiwaelemea mahasimu wao katika kipindi kikubwa cha mechi.
Mchezo wa fainali kati ya Senegal na Algeria ulichezwa katika uwanja wa soka wa kimataifa wa Cairo, wakati uwanja ulifurika huku mashabiki mbali wakijitokeza kwa wingi kuja kuzishajiisha timu hizo.
Mwandishi wa VOA aliyeko Cairo amesema kuwa wakati wakiwa bado nje ya uwanja kuna mamia ya mashabiki waliokosa tiketi za kuingia uwanjani kwa sababu mpaka inafika jana tiketi zote zilishanunuliwa.
Mwanahabari huyo pia amesema akiwa jijini Cairo alipata kuzungumza na baadhi ya mashabiki waliokosa tiketi ambao ni raia wa Saudia Arabia.
Naye raia wa Misri aliefanikiwa kuingia kwa tiketi ya wadhamini, mapema masaa machache kabla ya mechi kuanza, shabiki huyo aliiambia VOA kwamba mashirika mengi ambayo ni wadhamini kwenye michuano hii walizinunua tiketi kwa wingi na kuzigawa mapema kwa watu mbali mbali wengi wao wafanyakazi wa mashirika hayo.
Ndani ya uwanja mashabiki ambao ni wananchi wa Misri waligawanyika makundi mawili wengi wao wakiishabikia timu ya taifa ya Senegal na waliosalia timu ya taifa ya Algeria.
Imetayarishwa na Waandishi wetu, Cairo, Misri
AFCON 2019 MISRI :Ufafanuzi juu ya hatma ya kocha wa Tanzania
Rais wa TFF Tanzania atoa ufafanuzi juu ya kuondoka kwa kocha wa timu ya taifa ya Tanzania baada ya timu yake kutolewa katika michuano ya AFCON.
AFCON 2019 MISRI : Mahojiano Maalum
Mjumbe wa kamati ya utendaji ya CAF Leodger Tenga
AFCON 2019 MISRI : Wasemavyo wachambuzi juu ya Nigeria, Tunisia

Ni Jumatano ya kukata na shoka ambapo kuna mengi ya kutegemea kutokea kwenye mechi ya mshindi wa tatu ndani ya uwanja wa soka wa Al Salaam, ambapo Nigeria na Tunisia watachuana dimbani hapo ifikapo saa tatu kamili jioni kwa majira ya Cairo nchini Misri.
Asemavyo Leodger Tenga
Wachambuzi wa soka wanasema mechi ya fainali kati ya Senegal na Algeria itakuwa ngumu sana kwa sababu Algeria na ubavu wake wote tangu mwaka 1990 inataka kulichukua kombe hili tena ikiwa ni mara ya pili endapo wataishinda Senegal.
Na kwa upande wa timu ya taifa ya Senegal nayo inataka kuandika historia ya kunyakua kombe la AFCON mwaka 2019, na kuwekwa kwenye rekodi kama taifa bingwa barani Afrika japo watamkosa mchezaji wao muhimu kiungo wa kati Kalidou Koulibaly ambaye alipewa kadi mbili za njano katika mechi zilizopita ndani ya michuano hii.
Idhaa ya kiswahili ya Sauti ya Amerika (VOA) imemnukuu Mjumbe wa kamati ya utendaji ya CAF Leodger Tenga kwenye mazungumzo aliyofanya na Mwanahabri wetu Sunday Shomari jijini Cairo – akisema “ Koulibaly ni mchezaji mzuri hata ukimuona uchezaji wake …. kwa hiyo mimi ningefurahi kumuona, kwa sababu nataka wachezaji wazuri kabisa duniani wawepo kwenye fainali”.
Mshindi wa tatu
Kwa upande wa mchezaji John Obi Mikel mechi hiyo ndio itakuwa ya mwisho, ambapo ataagwa kiuchezaji, kwani ndio anastaafu kuchezea timu yake ya taifa ya Nigeria.
Mechi ya fainali
Kiwanja cha soka cha kimataifa cha Cairo ndani ya wiki hii kinahodhi mechi ya mwisho ya michuano ya AFCON 2019 ambayo ni mchezo wa fainali kati ya Senegal na Algeria ijumaa tarehe 19 Julai.
Mpaka muda huu vyombo vya usalama vimeshajipanga kiulinzi zaidi na mashabiki wa pande zote mbili nao wako tayari kufurika uwanjani.
Maandalizi
Hii ni ishara ya kuwepo maandalizi ya mchezo huo dimbani kama ilivyokuwa katika siku ya ufunguzi wa michuano hii ya AFCON 2019 tarehe 21 June au shamra shamra zake zikawa zaidi kuliko siku hiyo ya ufunguzi kutokana na kishindo cha fainali.
Imetayarishwa na mwandishi wetu, Cairo, Misri
AFCON 2019 MISRI : Mashabiki wa Algeria wakifurahia ushindi
Mitaa ya Cairo ilikuwa imefurika mashabiki wa timu ya Algeria wakisheherekea ushindi wao baada ya kuifunga Nigeria 2-1.
AFCON 2019 MISRI : Mashabiki wa Algeria wakifurahia ushindi
Mashabiki wa Algeria waonyesha umoja katika kusheherekea timu yao wakati ikicheza Jumapili. Algeria iliifunga Nigeria 2-1.
AFCON 2019 MISRI : Ghana VS Tunisia
Tunisia yaingia semifainali baada ya kuitoa Ghana
AFCON 2019 MISRI : Senegal VS Benin
Senegal yaingia semifainali kwa kuitoa Benin
AFCON 2019 MISRI : Nigeria yaifunga Afrika Kusini 2-1
Washabiki wa Nigeria watamba baada ya kuifunga Afrika Kusini
AFCON 2019 MISRI : Pambano la Madagascar, DRC
Timu ya Madagascar yaingia robo fainali katika mechi iliyochezwa Jumatatu.
AFCON 2019 MISRI : Viongozi wa chama cha soka Misri wajiuzulu

Rais wa chama cha soka cha Misri Hani Abou Rida amejiuzulu na kikosi kizima chaufundi kufuatia kutolewa kwa timu hiyo kusikotarajiwa katika michuano ya soka ya kombe la mataifa ya Afrika nchini Misri.
Kwa mujibu wa AFP uamuzi huo ni wa kutimiza ni wa haki na wajibu ilisema taarifa ya chama cha soka nchini Misri baada ya kuwaangusha mashabiki. Akiongeza kwamba wajumbe wote wa bodi wameombwa kujiuzulu.
Matokeo ya mechi ya Jumamosi yalipelekea mshtuko mkubwa kwa mashabiki wapatao 75,000 katika uwanja wa Cairo pamoja na wananchi wa Misri kwa jumla wakishuhudia timu yao iliyokuwa ikipewa nafasi kubwa ikiangushwa kwa bao 1-0 na Afrika kusini.
Rida ameongoza chama cha soka cha Misri tangu tangu mwaka 2016, katika muda wote chama hicho kimegubikwa na misukosuko ikiwa ni pamoja na timu kutolewa mapema katiika michuano ya kombe la dunia 2018 katika hatua ya makundi.
Uwanja wa soka wa kimataifa wa Cairo uliokuwa umefurika watu na ngoma na matarumbeta yalikuwa kimya kabisa baada ya mchezo huo huku baadhi ya washabiki wakibubujikwa na machozi ya kutoamini kilichotokea.
Wengi waliduwaa na kutoka nje ya uwanja kwa muda wakiwa wanashangaa na wengine wachache wakimpigia makofi na kumtaja golikipa mahiri wa timu hiyo Ahmed El Shenawi anayechezea timu ya Al Ahly.
Imetayarishwa na mwandishi wetu Sunday Shomari, Cairo, Misri
AFCON 2019 MISRI : Hali ilivyokuwa mchezo wa Afrika Kusini, Misri
Maelfu ya wapenzi wa soka nchini Misri wajitokeza katika pambano la Afrika Kusini na Misri.
AFCON 2019 : Uganda yaishukuru Afrika Mashariki kwa kuwaunga mkono
Mchezaji wa kimataifa wa Uganda Emmanuel Okwi, amewashukuru wana Afrika Mashariki kwa kuinga mkono timu ya Uganda na kuwa moyo wakati wote wa michuano hiyo.
AFCON 2019 MISRI : Mchezaji wa Kimataifa Sadio Mane Aisifu Uganda
Senegal iliwanyuka Uganda moja bila katika pambano lililokuwa kali la mtoano wa raundi ya 16 ya michuano ya AFCON. "Kusema kweli sijawahi kuona timu yenye stamina na washambuliaji hodari kama Uganda," ameeleza nyota wa timu ya Senegal Sadio Mane.