Balozi za Marekani katika nchi kadhaa zilikabiliwa na waandamanaji, walioghadhibishwa na kifo cha George Floyd kilichotokea Mei 25. Floyd alifariki baada ya polisi mzungu kuweka goti lake kwenye shingo lake kwa takriban dakika 9.
Dunia yalaani kifo cha Mmarekani mweusi akishikiliwa na polisi
Maandamano yamefanyika katika miji mbalimbali duniani Jumamosi, ikiwa ni mshikamano wa namna fulani na waandamanaji wa Marekani kufuatia kifo cha Mmarekani mweusi wakati akiwa mikononi mwa polisi mapema wiki hii.

1
Picha zinazoonyesha upande mmoja maandamano ya amani na upande mwengine uhalifu.

2
Watu, wengine wakiwa wamepiga magoti wamekusanyika Uwanja wa Trafalgar Square katikati ya mji wa London Jumamosi, Mei 31, 2020.

3
Watu wakiandamana Berlin, Ujerumani, Jumapili, Mei 31, 2020 dhidi ya ubaguzi against racism na uvunjifu wa sheria unaofanywa na polisi baada ya kifo cha kikatili cha Mmarekani mweusi George Floyd chini ya mikono ya polisi mzungu Marekani. (Bernd von Jutrczenka/dpa via AP)

4
Waandamanaji wakiwa mbele ya Ubalozi wa Marekani nchini Copenhagen, Denmark, Jumapili, May 31, 2020. Wakilaani kifo cha George Floyd, 46, chini ya mikono ya polisi huko Minneapolis, Marekani. (Ida Guldbaek Arentsen/Ritzau scanpix via AP)