Balozi za Marekani katika nchi kadhaa zilikabiliwa na waandamanaji, walioghadhibishwa na kifo cha George Floyd kilichotokea Mei 25. Floyd alifariki baada ya polisi mzungu kuweka goti lake kwenye shingo lake kwa takriban dakika 9.
Dunia yalaani kifo cha Mmarekani mweusi akishikiliwa na polisi
Maandamano yamefanyika katika miji mbalimbali duniani Jumamosi, ikiwa ni mshikamano wa namna fulani na waandamanaji wa Marekani kufuatia kifo cha Mmarekani mweusi wakati akiwa mikononi mwa polisi mapema wiki hii.

5
Waandamanaji wakiwa mbele ya Ubalozi wa Marekani mjini Berlin, Ujerumani Jumapili, May 31, 2020. Wakilaani kifo cha George Floyd, 46, chini ya mikono ya polisi huko Minneapolis, Marekani.

6
Waandamanaji Marekani wakikabiliana na mabomu ya machozi walipokuwa wakilaani kifo cha George Floyd akiwa mikononi mwa polisi, Washington, Marekani, Mei 30, 2020. REUTERS/Yuri Gripas

7
Picha za George Floyd, mtu aliyekuwa amefungwa pingu na kufariki baada ya kupelekwa rumande, Minneapolis, zikiwa zimetundikwa nje ya senyenge ya ubalozi wa Marekani mji wa Mexico City, Saturday, May 30, 2020.

8
Maandamano mjini Washington DC : Maji, baking soda na maziwa, yameachwa njiani kuwasaidia watu kuondoa athari za mabomu ya machozi yanayotupwa na jeshi la polisi.