Hatua hiyo inafuatia kujiuzulu Jumamosi kwa Mkuu wa Polisi wa mji wa Atlanta Erika Shields, baada ya Rayshard Brooks, umri miaka 27, kuuawa Ijumaa, na kusababisha wimbi jipya la maaandamano mjini Altanta baada ya kuwepo maandamano makubwa yakulaani kifo cha George Floyd akiwa chini ya ulinzi wa polisi huko Minneapolis yaliyokuwa yamepungua kasi.
Ghasia, maandamano yazuka Atlanta baada ya kifo cha mtu mweusi
Afisa wa polisi mjini Atlanta afukuzwa kazi baada ya kupiga risasi iliyosababisha kifo cha mtu mweusi na afisa mwengine amepangiwa kazi nyingine za kiutawala, idara ya polisi imetangaza mapema Jumapili

1
Mgahawa wa Wendy’s unawake moto kufuatia maandamano ya kupinga ubaguzi wa rangi na kitendo cha kuuawa Rayshard Brooks wakati akishikiliwa na polisi.

2
Picha hii iliyotolewa na Idara ya Polisi ya Atlanta inamuonyesha Rayshard Brooks akiongea na Afisa Garrett Rolfe kwenye eneo la kuengesha magari la mgahawa wa Wendy, Jioni Ijumaa, Juni 12, 2020, mjini Atlanta. (Atlanta Police Department via AP)

3
Gari ya Brooks iliyokuwa imepaki katika mgahawa wa Wendy.

4
Waandanamaji wakusanyika nje ya mgahawa wa Wendy's, Atlanta Jumamosi, Juni 13, 2020, Steve Schaefer/