Rais Magufuli amesema Benjamin William Mkapa amefariki dunia hospitalini Jijini Dar es Salaam ambako alikuwa akipatiwa matibabu.
Rais Magufuli amewataka Watanzania kuwa watulivu na wastahimilivu baada ya kupokea taarifa za kuondokewa na mpendwa wao Benjamin William Mkapa.
“Kwa masikitiko makubwa tumepata msiba mkubwa, Mzee wetu Benjamin William Mkapa, Rais Mstaafu wa Awamu ya Tatu amefariki dunia, amefariki dunia katika hospitali Jijini Dar es Salaam ambako alikuwa amelazwa, niwaombe Watanzania tulipokee hili, tumepata msiba mkubwa na tuendelee kumuombea Mzee wetu Rais Mstaafu Benjamin William Mkapa ambaye ametangulia mbele za haki, taarifa zingine zitaendelea kutolewa lakini Mzee Mkapa hatunaye tena” amesema. Rais Magufuli katika taarifa yake kwa Taifa.
Yafuatayo ni matukio muhimu yaliyoko katika kumbukumbu ya mahusiano yake na viongozi wa ulimwengu na nafasi yake kama mwanadiplomasia...
HAYATI BENJAMIN MKAPA : SAFARI NDEFU YA MWANADIPLOMASIA
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, John Pombe Magufuli ametangaza kifo cha Rais Mstaafu wa Awamu ya Tatu, Benjamin William Mkapa kilichotokea usiku wa kuamkia tarehe 24 Julai, 2020.

9
Ras Mkapa alipokutana na naziri wa mambo ya nje wa Marekani Warren Christopher mjini Dar es Salaam, Octoba 11, 1996.

10
Rais Mkapa na Katibu Mkuu wa UN Koffi Annan mjini Nairobi, Octoba 11, 2012.

11
Rais Kibaki na kiongozi wa upinzani Odinga waqtia saini makubaliano ya kugawana madaraka Februari 28, 2008.

12
Le facilitateur du dialogue inter-burundais, l’ancien président tanzanien Benjamin William Mkapa, accueilli par le ministre Burundais des relations extérieures, à son arrivée à Bujumbura, Burundi, 7 décembre 2016. (VOA/Chrsitophe Nkurunziza)