Siku ya Jumamosi Septemba 11, 2021, Wamarekani kwa mara nyingine wanawaenzi wahanga 2,977 wa mashambulizi ya Septemba 11, 2001, na familia zao, na wale pia waliojeruhiwa na waokoaji.
Kumbukumbu ya shambulizi la Septemba 11
Kumbukumbu hiyo ilifunguliwa katika eneo la maghorofa pacha ya World Trade Center. Makumbusho hayo yamejengwa katika eneo la moja ya maghorofa hayo na kufunguliwa Septemba 11, 2011, ili umma uweze kutembelea . Inawaenzi wale wahanga wote wa shambulizi la Septemba 11, 2001.

1
Eneo la south reflecting pool la Kumbukumbu ya Septemba 11 Memorial Plaza linaonekana katika maadhimisho ya miaka 10 ya kukamilika juhudi za awali za kusafisha eneo la tukio (Ground Zero) lilipoanzia huko New York, Mei 30, 2012. REUTERS/Andrew Burton

2
Wardi likiwekwa katika nakshi ya jina lililoandikwa katika eneo la South reflecting pool kwenye eneo la kumbukumbu - Ground Zero - katika hafla iliyotengwa rasmi kwa ajili ya Makumbusho ya Kumbukumbu ya Kitaifa ya Septemba 11 New York, Mei 15, 2014.

3
Kumbukumbu na Makumbusho ya Septemba 11, iliyopigwa picha katika eneo la maghorofa pacha yaliyoshambuliwa, New York, Aprili 23, 2021. Jengo refu limekalia pale yalipokuwa maghorofa pacha (Twin Towers) katika anga la New York. Ghorofa la One World Trade Center, lililofunguliwa 2014, limekuwa ni alama ya taifa la Marekani kujizatiti tena baada ya shambulizi la kutisha la Septemba 11.

4
Eneo la south pool la Kumbukumbu ya Septemba 11 linaonekana huku watalii wakitembelea ground zero huko New York Juni 5, 2012.