Siku ya Jumamosi Septemba 11, 2021, Wamarekani kwa mara nyingine wanawaenzi wahanga 2,977 wa mashambulizi ya Septemba 11, 2001, na familia zao, na wale pia waliojeruhiwa na waokoaji.
Kumbukumbu ya shambulizi la Septemba 11
Kumbukumbu hiyo ilifunguliwa katika eneo la maghorofa pacha ya World Trade Center. Makumbusho hayo yamejengwa katika eneo la moja ya maghorofa hayo na kufunguliwa Septemba 11, 2011, ili umma uweze kutembelea . Inawaenzi wale wahanga wote wa shambulizi la Septemba 11, 2001.

5
Maafisa wa polisi wako nje ya eneo la Ground Zero asubuhi ya maadhimisho ya miaka 15 ya mashambulizi ya Septemba 11 huko Manhattan, New York, Marekani, Septemba 11, 2016. REUTERS/Andrew Kelly

6
Wasafiri wakipita katika kituo cha usafiri cha Oculus huko New York, Julai 30, 2021. Paa la jengo hilo hufunguliwa kila Septemba 11 ikiwa ni kuwaenzi wahanga wa mashambulizi ya Septemba 11.

7
Kituo cha usafirishaji cha Oculus Kiko pembeni ya Mnara wa Uhuru mjini New York, Julai 30, 2021.

8
Hii picha inaonyesha ghorofa refu la One World Trade Center huko New York siku ya Julai 3, 2016, ni jengo refu lilikalia mahali palipokuwa maghorofa pacha (Twin Towers) katika anga za New York. Lilifunguliwa 2014.