Mahakama ya Ulaya, Jumatano hii imetupilia mbali pingamizi iliyofunguliwa na chombo cha habari cha serekali ya Russia, RT France.
RT ilifungua kesi dhidi ya marufuku iliyowekwa na Umoja wa Ulaya ya kutofanya shughuli zake.
Mahakama ya haki ya Ulaya ya Luxembourg imesema EU ilikuwa na uwezo wa kusimamisha shughuli za RT France, na vikwazo vya EU havikutaja shauri hilo kama la uhuru wa maoni.
Msemaji wa Kremlin, Dmitry Peskov, aliwaambia wanahabari kwamba Russia itachukuwa uamuzi kama huo kutoa msukumo kwa vyombo vya habari vya magharibi ambavyo vinafanyakazi ndani ya Russia.
EU iliweka vikwazo na marufuku mwezi Machi, ikisimamisha shughuli za RT English, RT –UK, RT Germany, RT France na RT Spanish.