Rais Bush alifariki dunia siku ya Ijumaa iliyopita akiwa na umri wa miaka 94, takriban miezi minane baada ya kufa mkewe Barbara Bush. (AP Photo/Robert F. Bukaty)
Matayarisho ya maziko ya Rais mstaafu George H.W. Bush
Matayarisho ya maziko ya Rais mstaafu George H.W. Bush yakiendelea huko Texas kabla ya mwili wake kuletwa jijini Washington, DC, Marekani.

1
Rais mstaafu wa Marekani George H. W. Bush alifariki siku ya Ijumaa iliyopita huko Texas, Marekani

2
Kikosi maalum cha kumlinda Rais wa Marekani wakiwa wamebeba jeneza la Rais mstaafu George H.W Bush katika nyumba ya kutayarisha maiti baada ya familia kufanya maombi, Jumatatu, Desemba 3, 2018, huko Houston. Jumatatu, Desemba 3, 2018, huko mjini Houston. (AP Photo/Kiichiro Sato)

3
Rais Donald Trump akizungumza na vyombo vya habari juu ya kifo cha Rais mstaafu George H. W. Bush, wakati alipokutana na Chansela wa Ujerumani Angela Merkel katika mkutano wa G20, Jumamosi, Desemba 1, 2018, huko Buenos Aires, Argentina. (AP Photo/Pablo Martinez Monsivais)

4
Chansela wa Ujerumani Angela Merkel akizungumza na vyombo vya habari juu ya kifo cha Rais mstaafu George H.W. Bush wakati alipokutana na Rais Donald Trump, katika mkutano wa G20, Jumamosi, Desemba 1, 2018, huko Buenos Aires, Argentina.(AP Photo/Pablo Martinez Monsivais)