Rais Obama aitembelea Kenya (1)
Rais Obama aitembelea Kenya (1)

9
Kikosi cha bendi ya jeshi la anga la kenya kabla ya kuwasili kwa Rais wa Marekani, Barack Obama kwenye ikulu mjini Nairobi, Jumamosi, July 25, 2015. Rais Obama amelitaja bara la Afrika linasonga mbele, akiwa nchini Kenya Jumamosi, katika taifa la Afrika Mashariki ambalo ana uhusiano nalo mkubwa wa kifamilia.

10
Msichana Joan Wamaitha mwenye umri wa miaka nane, akimlaki Rais Barack Obama kwa maua alipowasili kwenye uwanja wa ndege wa kimataifa wa Kenyatta, Ijumaa, Julai 24, 2015, huko Nairobi, kenya. Obama ni rais wa kwanza wa Marekani aliyepo madarakani kuitembelea Kenya, sehemu ambako baba yake amezaliwa.

11
Rais Barack Obama anashiriki katika mkutano wa pamoja na Rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta huko Ikulu, Jumamosi, Julai 25, 2015, mjini Nairobi, Kenya.

12
Rais Barack Obama, kulia, akipeana mikono na Rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta kabla ya mkutano wa pamoja huko Ikuly, Jumamosi, Julai 25, 2015, mjini Nairobi, Kenya.