Marais wa nchi tisa za Afrika ni miongoni mwa wageni mashuhuri waliohudhuria shughuli ya kitaifa ya kumuaga aliyekuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Hayati, John Pombe Magufuli jijini Dodoma Jumatatu. Picha zote na Ofisi ya Rais.
Rais Samia aongoza viongozi wa mataifa kuuaga mwili wa Hayati Magufuli
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan, akiongoza Viongozi wa Mataifa ya Nchi mbalimbali Duniani na Wananchi wa Jiji la Dodoma kwenye Mazishi ya Kitaifa ya kuuaga Mwili wa hayati Rais John Pombe Magufuli katika Uwanja wa Jamhuri JIjini Dodoma leo March 22,2021.

1
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan akitoa heshima za mwisho kwenye jeneza lenye mwili wa aliyekuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika awamu ya tano hayati John Pombe Magufuli katika uwanja wa Jamhuri Dodoma. Picha na Ofisi ya Rais.

2
Rais wa Zanzibar Hussein Ali Mwinyi akitoa heshima za mwisho kwenye jeneza lenye mwili wa aliyekuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika Awamu ya tano Hayati John Pombe Magufuli katika uwanja wa Jamhuri mkoani Dodoma. Picha na Ofisi ya Rais.

3
Rais wa Jamhuri ya Watu wa Kenya Uhuru Kenyatta akitoa heshima za mwisho kuuaga Mwili wa aliyekuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania hayati John Pombe Magufuli kwenye mazishi ya kitaifa yaliyo fanyika leo Machi 22, 2021, Dodoma.

4
Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC Felix Tshisekedi akitoa heshima za mwisho kwenye jeneza lenye mwili wa aliyekuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika awamu ya tano Hayati John Pombe Magufuli katika uwanja wa Jamhuri Dodoma.