Marais wa nchi tisa za Afrika ni miongoni mwa wageni mashuhuri waliohudhuria shughuli ya kitaifa ya kumuaga aliyekuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Hayati, John Pombe Magufuli jijini Dodoma Jumatatu. Picha zote na Ofisi ya Rais.
Rais Samia aongoza viongozi wa mataifa kuuaga mwili wa Hayati Magufuli
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan, akiongoza Viongozi wa Mataifa ya Nchi mbalimbali Duniani na Wananchi wa Jiji la Dodoma kwenye Mazishi ya Kitaifa ya kuuaga Mwili wa hayati Rais John Pombe Magufuli katika Uwanja wa Jamhuri JIjini Dodoma leo March 22,2021.

9
Gari Maalumu la Jeshi la Wananchi wa Tanzania JWTZ likiwa limebeba Jeneza lenye mwili wa aliyekuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika awamu ya tano Hayati John Pombe Magufuli wakati likiwasili katika uwanja wa Jamhuri mkoani Dodoma.