Makombora mawili ya angani yaliyokuwa yakiongozwa na Kinzhal yaliharibiwa na mifumo ya ulinzi wa anga ya Ukraine, kwa mujibu wa jeshi la anga, na kuongeza kuwa pia lilitungua ndege tatu za upelelezi za Russia.
Katika wiki za hivi karibuni, Russia, imeongeza kwa kiasi kikubwa idadi ya mashambulizi ya makombora na ndege zisizo na rubani kwenye miundombinu ya nishati ya Ukraine huku akiba ya mifumo ya ulinzi wa anga na risasi za Ukraine ikipungua, na kusababisha idadi kubwa ya vifo vya raia na uharibifu mkubwa.
Wakati huo huo, Wizara ya Ulinzi ya Russia, imesema mifumo yake ya ulinzi wa anga ilitungua ndege 50 za Ukraine zisizo na rubani katika mikoa minane ya Russia, Aprili 20.
Forum