Makubaliano hayo yalisainiwa Jumatatu na Rais wa mpito Ahmad al-sharaa na Mazloum Abdi, Kamanda wa kundi la waasi wa Kikurdi wanaoungwa mkono na Marekani.
Makubaliano hayo yanaashiria mafanikio makubwa ambayo yataiweka sehemu kubwa ya Syria chini ya udhibiti wa serikali inayoongozwa na kundi lililoongoza uasi wa kumuondoa madarakani Rais Bashar Assad mwezi Disemba.
Makubaliano hayo yatakayotekelezwa mwishoni mwa mwaka huu yatarejesha maeneo yote ya mpaka na Iraq na Uturuki huko kaskazini mashariki, viwanja vya ndege na maeneo ya mafuta chini ya udhibiti wa serikali kuu.
Wakurdi watapewa tena haki zao ikiwemo kufundisha na kuzungumza lugha yao, haki ambazo zilikuwa zimepigwa marufuku kwa miongo kadhaa chini ya utawala wa Assad.
Forum