Sherehe hizo zimefanyika chini ya ulinzi mkali na imara nje ya ngazi za Bunge la Marekani, Washington, Januari 20, 2021.
Sherehe za kuapishwa Rais Joe Biden na Makamu Rais Kamala Harris
Joe Biden ameapishwa Jumatano kuwa Rais wa 46 wa Marekani pamoja na Makamu Rais Kamala Harris, Seneta wa zamani Baraza la Seneti la Marekani.

1
Joe Biden akiapa kuwa rais wa 46th wa Marekani mbele ya Jaji Mkuu John Roberts huku mkewe Jill Biden akishikilia Bibilia nje ya Jengo la Bunge la Marekani.

2
Rais Joe Biden akihutubia baada ya Kula kiapo nje ya Congress, Washington, Jumatano, Jan. 20, 2021.(AP Photo/Patrick Semansky, Pool)

3
Rais mteule Joe Biden, mkewe Jill Biden na Makamu Rais mteule Kamala Harris na muwewe Doug Emhoff wakiwasili Bungeni kwa ajili ya sherehe rasmi za kuapishwa mjini Washington, Jumatano, Jan. 20, 2021. (AP Photo/J. Scott Applewhite)

4
Kamala Harris akiapishwa kuwa Makamu Rais na Jaji wa Mahakama ya Juu Sonia Sotomayor huku mumewe Doug Emhoff akishikilia Bibilia Washington, Jumatano, Jan. 20, 2021. (AP Photo/Patrick Semansky, Pool)