Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Mei 05, 2025 Local time: 02:02

Sintofahamu Sudan kusini: Wanajeshi wamezingira makao ya Machar


Rais wa Sudan kusini Salva Kiir akihutubia waandishi wa habari. Nyuma yake, upande wa kulia ni makam wake Riek Machar. Februari 20, 2020. PICHA: AFP
Rais wa Sudan kusini Salva Kiir akihutubia waandishi wa habari. Nyuma yake, upande wa kulia ni makam wake Riek Machar. Februari 20, 2020. PICHA: AFP

Wanajeshi wa Sudan kusini wamezingira makao ya makam rais Riek Machar katika mji mkuu wa Juba.

Washirika wa karibu kadhaa wa Machar wamekamatwa.

Machar, ambaye uhasama wake wa kisiasa na rais Salva Kiir umepelekea vita vya wenyewe kwa wenyewe, alisema mwezi uliopita kwamba hatua ya rais Kiir kufuta kazi washirika wake wa karibu kutoka serikalini, inatishia makubaliano ya amani yam waka 2018 kati yake na Kiir, yaliyomaliza viya vya wenyewe kwa wenyewe vya miaka 5, vilivyosababisha vifo vya zaidi ya watu 400,000.

Naibu wa mkuu wa jeshi la Sudan kusini Generali Gabriel Duop Lam, ambaye pia ni mshirika wa Machar, alikamatwa na kuzuiliwa Jumanne, akihusishwa na mapigano ya kaskazini.

Waziri wa mafuta Puot Kang Chol, ambaye pia ni mshirika wa Machar, Pamoja na walinzi wake na familia nao wamekamatwa na kuzuiliwa.

Hakuna sababu imetolewa kuhusu hatuaya kukamatwa kwao.

Machar na chama chake cha SPLM-IO, hawajatoa taarifa yoyote kuhusu mapigano yanayoendelea, lakini Waziri wa maji Pau Mai Deng, ambaye pia ni msemaji wa chama, amesema kukamatwa kwa Lam ‘kunatishia makubaliano ya amani kwa jumla.”

Wanadiplomasia wa nchi za magharibi walitoa wito kwa pande zote kuepusha uhasama.

Sudan kusini haijatekeleza mkapata wa amani wa mwaka 2018 kwa ukamilifu. Uchaguzi uliokuwa umepangiwa kufanyika mwaka uliopita uliahirishwa kwa muda wa miaka miwili kutokana na ukosefu wa pesa.

Kufutwa kazi kwa makam rais 2

Mwezi Februari, rais Kiir alifuta kazi makam rais wawili, mkuu wa ujasusi na maafisa wengine wa ngazi ya juu serikalini.

Hatua ya maafisa hao kufutwa kazi ilitangazwa kupitia shirika la habari la serikali. Hakuna sababu ilitolewa.

Sudan kusini ina makar ais 5 kama sehemu ya makubaliano ya amani ya mwaka 2018.

Sudan kusini, yenye utajiri mkubwa wa mafuta, iliundwa kutoka kwa Sudan mwaka 2011, lakini imekumbwa na vita vya wenyewe kwa wenyewe baada ya rais Kiir na makam wake Riek Machar kukosa kuelewana.

Utekelezaji wa makubaliano ya amani ya mwaka 2018 umekumbwa na changamoto kadhaa.

Mmoja wa makam rais waliofutwa kazi mwezi Februari ni James Wani Iga, mwanasiasa wa muda mrefu na ambaye pia ni generali katika jeshi. Alishikilia nafasi hiyo tangu mwaka 2013 na alikuwa naibu mwenyekiti wa chama cha SPLM, chake rais Kiir.

Mwingine ni Hussein Abdelbagi Akol, kutoka muungano wa upinzani SSOA, ambao sio sehemu ya chama kikuu cha upinzani cha SPLM -IO, chake makam rais Riek Machar.

Akol aliteuliwa kuwa Waziri wa kilimo, akichukua nafasi ya Josephine Joseph Lagu, ambaye aliteuliwa kuwa makam rais.

Benjamin Bol Mel, ambaye aliwekewa vikwazo na Marekani mwaka 2017 kwa madai ya ufisadi, aliteuliwa kuwa makam rais.

Mel, ambaye alikuwa mjumbe wa rais Kiir katika usimamizi wa mipango maalum, ametajwa na wachambuzi kuwa anatayarishwa kumrithi rais Kiir.

Makubaliano ya amani yam waka 2018, yanampa mamlaka rais Kiir kuteua na kuwafuta kazi maafisa wa serikali kuu na za majimbo.

Anaweza kufuta na kuteua maafisa kutoka upinzani kwa ridhaa ya uongoz wa vyama hivyo.

Sudan kusini haijawahi kuandaa uchaguzi tangu ilipopata uhuru 2011.

Forum

XS
SM
MD
LG