Kiongozi wa Kikosi cha RSF -Sudan amewasili nchini Ethiopia katika kituo cha pili cha safari yake ya kwanza nje ya nchi tangu vita vilipozuka na jeshi la Sudan mwezi Aprili.
Ziara za Mohamed Hamdan Daglo nchini Ethiopia na Uganda zinakuja wakati wanadiplomasia wa kikanda wakihangaika kufanikisha mkutano kati ya kamanda wa RSF na mpinzani wake mkuu wa jeshi la Sudan Abdel Fattah al-Burhan.
Majenerali hao wanaopigana hawajakutana ana kwa ana tangu kuzuka kwa mapigano kati ya vikosi vyao ambayo yamesababisha vifo vya zaidi ya watu 12,000 kwa makadirio ya kihafidhina, na kulazimisha mamilioni kukimbia.