Geogina Kerubo wa kundi la Global Young Green anasema ni jukumu lao kama wanaharakati kuwaelimisha watu juu ya masuala ambayo ni muhimu yanayowahusu.
Maandamano yamefanyika wakati wajumbe wamekuwa wakijadili pendekezo kutoka nchi zilizoendelea kuongeza kiwango cha kugharimia athari za mabadiliko ya hali ya hewa kufikia dola bilioni 250 kutoka bilioni 100.
Viongozi wanawake wakiwa katika picha ya pamoja katika mkutano wa COP29, Alhamisi, Novemba 21, 2024, Baku, Azerbaijan.
Hata hivyo mataifa yanayoendelea wanasema kiwango hicho hakitoshi wakati wanahitaji hivi sasa dola trilioni 1.3 kugharimia athari hizo kufikia 2035.