Kiongozi mkuu wa Iran, na wawakilishi wa wanamgambo wa Palestina walilisalia jeneza la Ismail Haniyeh na mlinzi wake ambaye aliuawa katika mauaji ambayo Israel inalaumiwa kuhusika na kuna hatari ya kusambaa kwa vita katika kanda nzima.
Kiongozi wa Juu wa Kidini Iran Ayatollah Ali Khamenei akisalia jeneza la mkuu wa Hamas, Ismail Haniyeh, Tehran, Iran, Agosti 1, 2024.
Kituo cha televisheni cha serikali ya Iran baadaye kilionyesha majeneza yakiwekwa kwenye gari na kupitishwa mtaani kuelekea kwenye eneo la Azadi Square mjini Tehran na watu wakirusha maua kwenye majeneza hayo.
Baada ya ibada ya mazishi mjini Tehran, mwili wa Haniyeh unatarajiwa kupelekwa kwa maziko siku ya Ijumaa.
Habari hii inatokana na vyanzo mbalimbali vya habari.