Rais Donald Trump amesema mkutano wa Hanoi, Vitenam, kati yake na Kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong Un, Jumatano, umekuwa na mafanikio."Tulipiga hatua ya kutosha na nafikiri maendeleo makubwa kuliko yote ni maelewano yetu ambayo kwa kweli ni mazuri,” Trump amesema kumwambia Kim.
Mkutano wa Hanoi wajenga uhusiano mzuri kati ya Trump, Kim
Rais Trump akielezea nukta muhimu wakati akiwa na Mwenyekiti Kim katika mkutano wao huko Hanoi, Vietnam.
Trump akisalimiana na Kim
Rais Donald Trump na kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong Un kabla ya kuanza kikao cha watu wawili peke yao katika ukumbi wa hoteli huko Hanoi, Vietnam, Feb. 27, 2019.
Rais Donald Trump na Kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong Un wakiwa wanapata chakula cha usiku baada ya mkutano wao katika hoteli ya Metropole, Hanoi, Vietnam Feb. 27, 2019.
Watu hawa wakiwa karibu na ukumbi wa mkutano mjini Hanoi