Baada ya usiku kuingia, polisi wa kutuliza ghasia waliwakabili waandamanaji katika Chuo Kikuu cha New York na kuwakamata watu wengi.
Mamia ya waandamanaji walikaidi amri ya chuo kikuu kuondoka kwenye uwanja ambako walikusanyika.
Polisi wa New York wakimkamata mwanafunzi wa Kipalestina ambaye alikuwa amepiga kambi katika Chuo Kikuu cha New York ikiwa ni hatua ya kupinga vita kati ya Hamas na Israel. (Photo by Alex Kent / AFP)
Waandamanaji walikuwa wanadpiga kelele wakiitaka mamlaka ya Chuo Kikuu cha New York, NYU kuachana na juhudi zinazohusishwa na vita vya Israel huko Gaza.
Katika Chuo Kikuu cha Columbia cha New York, polisi waliwazuia waandamanaji kadhaa.
Polisi wakimkamata mwaandamanaji aliyepiga kambi katika Chuo Kikuu cha Columbia , Alhamisi, Aprili 18, 2024, huko New York. (Joshua Briz via AP)
Maandamano yanayoendelea katika vyuo vikuu ni taswira ya kuongezeka kwa mzozo kati ya Israel na Palestina, ulioanza tarehe 7 Oktoba kwa shambulio baya la wanamgambo wa Kiislamu wa Hamas nchini Israel, na jibu kali la Israel katika Gaza inayodhibitiwa na Hamas.