Zelenskyy aliandika kwenye ukurasa wake wa Twitter kwamba uharibifu wa bwawa hilo ulikuwa wa makusudi kabisa huku akiwalaumu wanajeshi wa Russia.
Rais pia ameishutumu Moscow zaidi kwa kutochukua hatua kusaidia wale wanaoishi katika maeneo yaliyo chini ya udhibiti wao ambao sasa wanakabiliana na athari za mafuriko.
Waokoaji wakiwaondoa watu katika eneo la mafuriko baada ya bwawa la Nova Kakhovka kulipuliwa, huko Kherson, Ukraine, Juni 7, 2023.
Maafisa wa Ukraine walisema zaidi ya watu 17,000 walikuwa wakihamishwa kutoka maeneo kando ya Mto Dnipro.
Wakati huo huo takriban miji na vijiji 40 vilikuwa vimefurika maji katika maeneo yaliyo chini ya udhibiti wa Ukraine kufuatia shambulizi hilo.
Mitaa ya Kherson, Ukraine yafurika maji Juni 7, 2023 baada ya kuta za bwawa hilo kubomoka.
Zaidi ya watu 900 walihamishwa kutoka maeneo yanayokaliwa na Russia.