CAG amesisitiza kuwa neno 'dhaifu' ni lugha ya kawaida katika ukaguzi wetu. na litaendelea kutumika.
kauli mbiu za kumbukumbu hii inasema “Isereje Kamwe Tena.” Suala la kuzuia mauaji ya halaiki yasitokee tena litazungumziwa wakati wa maadhimisho hayo.
“Sisi tunashirikiana vizuri kabisa,” Trump amesema akimsifia waziri mkuu huyo wa zamani wa Norway.
Baraza la kikatiba lenye wanachama 12 nchini Algeria linatarajiwa kufanya kikao chake Jumatano kuthibitisha hatua ya kujiuzulu kwa Bouteflika.
Kwa zaidi ya mwezi mmoja tangu mvutano kati ya nchi za Rwanda na Uganda kujulikana, hakuna mazungumzo ya pamoja yaliyofanyika kati ya nchi hizo mbili, wakati uongozi wa nchi hizo, kwa mapana zaidi, kila mmoja akishikilia msimamo wa uamuzi wa mkakati wake kushughulikia sintofahamu hii.
Takriban wananchi wa Gaza 200 wameuawa na vikosi vya Israeli tangu maandamano hayo yaanze, kwa mujibu wa takwimu za Wizara ya Afya ya Palestina,
“Tutaendelea kushikilia milima hiyo na hatutairejesha kamwe,” amesema Netanyahu.
Israel ilikamata eneo hilo lilioko upande wa kaskazini mashariki ya Syria wakati wa vita ya mwaka 1967, iliyodumu kwa situ sita na baadae kuendelea kulikalia eneo hilo mwaka 1981.
Msemaji wa White House Hogan Gidley amesema kuwa ofisi yao ilikuwa haijapokea na wala haijapewa muhtasari wowote juu ya ripoti hiyo.
Serikali ya Zimbabwe imesema imepeleka maombi kwa jumuiya ya kimataifa ipatiwe msaada wa madawa, chakula na ujenzi wa miundombinu, wakati waathirika wa kimbunga Idai wakishinikiza misaada hiyo kutumwa haraka iwezekanavyo. Kwa mujibu wa Umoja wa Mataifa wahanga wa janga hilo wamefikia 615.
Uchunguzi huo umepelekea kukutikana na makosa ya kujibu watu binafsi 37 na vikundi mbalimbali, wengi wao ni majasusi wa Russia ambao hawajakamatwa mpaka sasa.
Eneo la Golan Heights –...lilichukuliwa kwa nguvu na Israeli mwaka 1967 katika vita viliyodumu kwa siku sita.
Hadi Allhamisi asubuhi vifo 200 vimethibitishwa kutokea Msumbiji, zaidi ya 100 Zimbabwe na karibu 60 nchini Malawi. Mamia wamejeruhiwa na wengine wengi hawajulikani waliko.
Tanis amepangiwa kuhudhuria usikilizwaji wa kesi hiyo itakayofanyika faragha Ijumaa.
Kamishna wa polisi wa New Zealand Mike Bush amesema kuwa kutambua miili ilioyosalia na kuikabidhi kwa familia zao ili waweze kuandaa mazishi, inabakia kuwa ni kipaumbele chetu.
Mwenyekiti wa Chadema, Mkoa wa Arusha, Aman Golugwa, ameliambia gazeti la Mtanzania kuwa watapeleka vielelezo hivyo ili vyombo vya sheria vitafsiri uamuzi uliofanywa na Spika Ndugai.
Maalim Seif Shariff amesema Jumatatu anaridhia na maamuzi ya Mahakama Kuu kumtambua Ibrahim Lipumba, kuwa ndiye mwenyekiti wa Chama cha Wananchi CUF, anayetambuliwa na Msajili wa Vyama vya Siasa.
Kamishna wa Polisi nchini New Zealand Mike Bush amesema Jumapili kuwa mwili mmoja wa muhanga wa mauaji yaliyofanyika katika misikiti ya Ijumaa mjini Christchurch utaanza kukabidhiwa kwa familia ya marehemu kuanzia Jumapili usiku.
Tayari, shughuli za Forodha katika eneo la Gatun/Katuna zimezorota na kuendelea hivyo kwa nyakati zote, na magari tu madogo na baadhi ya mabasi machache yakipita mpakani.
Washukiwa wawili washiriki katika mauaji hayo pia wako chini ya udhibiti wa polisi.
Pandisha zaidi