Waziri Mkuu wa Haiti Ariel Henry amejiuzulu kama kiongozi wa taifa la Caribbean, kiongozi wa jumuiya ya kikanda na rais wa Guyana alisema Jumatatu usiku.
Raia mmoja wa Korea Kusini alikamatwa nchini Russia kwa madai ya ujasusi, shirika la habari la serikali ya Russia TASS liliripoti Jumatatu.
Mashambulizi ya anga yaliyotekelezwa na muungano wa jeshi la Marekani na Uingereza yalilenga miji ya bandari na miji midogo magharibi mwa Yemen Jumatatu, na kuua watu 11 na kujeruhi wengine 14, msemaji wa serikali ya Yemen inayotambuliwa kimataifa ameliambia shirika la habari la Reuters.
Jenerali wa juu wa kijeshi kutoka jeshi la Sudan amefuta uwezekano wa sitisho la mapigano katika mwezi mtukufu wa Ramadan, mpaka pale kundi la kijeshi linalo pigana na serikali litakapo ondoka kwenye maeneo ya raia na umma.
Ukraine Jumapili ilipinga wito wa Papa Francis wa kujadili kusitisha vita na Russia, huku Rais Volodymyr Zelenskiy akisema Papa alikuwa akifanya “upatanishi kwa mbali” na waziri wake wa mambo ya nje akisema Kyiv haitasalimu amri.
Waziri mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu Jumapili alisema kwamba magaidi wasiopungua 13,000 ni miongoni mwa Wapalestina waliouawa katika vita vya Israel dhidi ya Hamas katika Ukanda wa Gaza na ameapa kuendeleza mashambulizi kusini mwa eneo hilo.
Mtoto wa kiume wa mkuu wa jeshi la Sudan Abdel Fattah al-Burhan amejeruhiwa vibaya katika ajali ya barabarani nchini Uturuki, ripoti ya chombo cha habari nchini humo imesema.
Ufaransa itabakisha wanajeshi wake nchini Chad, iliyo chini ya utawala wa kijeshi, huku ikiwaondoa kwingineko barani Afrika, kutokana na mvutano na tawala za kijeshi, mjumbe wa Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron alisema Alhamisi.
Tajiri mkubwa sana barani Afrika kutoka Nigeria Aliko Dangote, anapanga kufungua ofisi ya mauzo ya bidhaa za mafuta, ikitarajiwa huenda ikafunguliwa h mjini London, ili kusaidia kuendesha soko la mafuta na bidhaa kutoka kwenye kiwanda chake kipya cha kusafisha mafuta.
Polisi nchini Kenya wamesema Jumanne, kwamba watu wawili wamekufa kwenye ajali kati ya ndege ya chuo cha urubani, na ile ya abiria, kwenye mji mkuu wa Nairobi.
Mswaada dhidi ya ushoga nchini Ghana unaweza kusababisha nchi hiyo kupoteza dola bilioni 3.8 ufadhili kutoka Benki ya Dunia kwa kipindi cha miaka mitano mpaka sita.
Makamu Rais wa Marekani Kamala Harris Jumapili alitoa wito wa sitisho la mara moja la mapigano katika ukanda wa Gaza na kuishinikiza kwa dhati Israel kuongeza usambazaji wa misaada ili kupunguza kile alichokiita “hali isiyo ya kibinadamu” na “janga la kibinadamu” miongoni mwa Wapalestina.
Zaidi ya watu bilioni 1 duniani sasa wanachukuliwa kuwa wanene kupita kiasi, hali inayohusishwa na ongezeko la hatari la matatizo mengi ya kiafya, kulingana na makadirio yaliyosahihishwa na kundi la watafiti wa kimataifa wa shirika la afya duniani (WHO).
Marekani Jumatano ilisema "imefadhaishwa mno" na kupitishwa kwa mswada wa sheria kali dhidi ya wapenzi wa jinsia moja, na bunge la Ghana, na kuhimiza utathminiwe upya, ili kubaini kama unafuata katiba ya nchi hiyo.
Takriban watu 576,000 katika Ukanda wa Gaza, robo ya wakazi wa Gaza wako katika hatari kubwa ya kukabiliwa na njaa, afisa mkuu wa Umoja wa mataifa aliliambia Baraza la usalama la Umoja wa mataifa Jumanne, akionya kwamba janga kubwa la njaa halitaepukika ikiwa hatua hazitachukuliwa.
Tume ya majadiliano ya kitaifa ya Senegal itapendekeza uchaguzi wa rais ulioahirishwa ufanyike tarehe 2 Juni huku Rais Macky Sall akisalia madarakani hadi mrithi wake atakapoapishwa, mjumbe wa tume hiyo Ndiawar Paye alisema Jumanne.
Rais wa Marekani Joe Biden amesema ana matumaini kuwa sitisho la mapigano katika mzozo kati ya Israel na Hamas huko Gaza litapatikana ifikapoJumatatu, wiki ijayo, huku pande zinazozozana zikionekana kukaribia kufikia makubaliano katika mazungumzo yanayofanyika nchini Qatar.
Hungary inatarajiwa kuiidhinisha Sweden kujiunga na NATO na kuondoa kizingiti cha mwisho kwa hatua ya kihistoria ya nchi hiyo ya Nordic ambayo taifa hilo lilionyesha usawa katika vita viwili vya dunia na mzozo uliopamba moto wa Vita Baridi.
Barabara za mji mkuu wa Guinea wa Conakry Jumatatu zimebaki tupu, na biashara kufungwa, kufuatia mgomo wa kitaifa wa wafanyakazi wakiwemo wachimba madini ,wakiitisha nyongeza za mishahara miongoni mwa mengine.
Papa Francis amelazimika kufuta mkutano na waumini leo Jumatatu asubuhi kwa sababu bado anasumbuliwa na flu, Vatican imesema katika taarifa yake.
Pandisha zaidi