Sebastien Haller alifunga bao la ushindi dakika tisa kabla ya mchezo kumalizika wenyeji Ivory Coast wakinyakua taji la tatu la Kombe la Mataifa ya Afrika kwa ushindi wa 2-1 dhidi ya Nigeria kwenye mchezo wa fainali Uwanja wa Alassane Ouattara mjini Abidjan Jumapili (Februari 11).
Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa alitumia hotuba yake bungeni siku ya Alhamisi, kuelezea mafanikio ya chama chake, katika miaka 30 iliyopita, lakini akatoa maelezo machache kuhusu mipango yake ya kushughulikia changamoto kuu zinazoendelea kuikumba nchi hiyo.
Mahakama ya Rufaa ya Serikali Kuu imetoa uamuzi kuwa Donald Trump hana kinga kwa mashtaka ya kuhusika na njama ya kubadilisha matokeo ya uchaguzi wa 2020 alioshindwa, ikimsogeza rais wa zamani wa Marekani karibu zaidi na kesi ya uhalifu ambayo haijawahi kutokea.
Bunge la Ethiopia limeongeza kwa miezi minne, muda wa kipindi cha hali ya dharura, iliyotangazwa mwezi Agosti, katika juhudi za kukabiliana na uasi katika eneo la kaskazini la Amhara, ambao unalaumiwa kwa kusababisha vifo vya mamia ya watu.
Fainali za Kombe la Dunia la mwaka 2026 zitafanyika kwenye Uwanja wa MetLife, katika jimbo la New Jersey, Marekani, waandaaji wa michuano hiyo, FIFA, walitangaza Jumapili.
Rais wa Namibia Hage Geingob alifariki dunia mapema Jumapili, wiki kadhaa baada ya kugunduliwa kuwa na saratani, afisi yake ilisema.
Huku vita kati ya wanamgambo wa Hamas na Israeli vikiingia mwezi wa nne, Waziri wa Mambo ya Nje wa Afrika Kusini amesema jumuiya ya kimataifa inapaswa kusitisha ufadhili kwa jeshi la Israeli.
Katikati ya mwezi Januari, katika mkusanyiko mdogo kwenye mji wenye kambi ya jeshi huko Myanmar, kiongozi wa kidini mwenye msimamo mkali anayeliunga mkono jeshi Pauk Kotaw alipendekeza kuwa mtawala wa kijeshi nchini Min Aung Hlaing kuachia madaraka na naibu wake kuongoza.