Seif Sharif ni mmoja kati ya viongozi wachache wa Afrika waloishi maisha ya kawaida bila ya kupenda makubwa. Ni kiongozi aliyependwa sana na wananchi kwa ustahmilivu wake na kutaka umoja wa wa-Zanzibari. Na anakua pia kiongozi wa upinzani aliyegombania kiti cha rais kwa miaka mingi bila ya kushinda.
Maisha ya kisiasa ya Maalim Seif Shariff Hamad kiongozi wa upinzani Zanzibar
- Abdushakur Aboud
Maalim Seif Shariff Hamad kiongozi wa upinzani wa Zanzibar kwa karibu miongo mitatu, afariki akiwa na umri wa miaka 77 baada ya kuugua ugonjwa wa Covid-19.

1
Seif Shariff mgombea wa CUF ahutubia kampeni kabla ya wafuasi wake kupambana na wa CCM 2005

2
Seif Shariff kiongozi wa upinzani akiwashukuru wafuasi wakati wa kampeni yake ya mwisho 2020

3
Seif Shariff kiongozi wa ACT akipiga kura wilaya ya Garagara, Zanzibar Oktoba 28, 2020

4
Maalim Seif Sharif akitoka ofisini kwake Stone Town baada ya kuachiliwa huru Oct 27, 2020