Maafisa wa uchaguzi wanasema kumekuwepo na wapigaji kura wengi walojitokeza katika uchaguzi unaofuatiliwa kwa karibu kupima mfumo wa kidemokrasia wa taifa hilo la Afrika Magharibi.
Wagambia wapiga kura kwenye uchaguzi wa rais
- Abdushakur Aboud
Kwa mara ya kwanza baada ya miaka 27 wananchi wa Gambia washiriki kwenye uchaguzi bila ya hofu kutokana na kutokuwepo na jina la kiongozi wa mabavu Yahya Jammeh.

5
Mpiga kura atoka kwenye kibanda cha kupiga kura mjini Banjul, Gambia

6
Mpiga kura aweka wino kwenye kidole baada ya kupiga kura mtaani Kanifing, Banjul

7
maafisa wa uchaguzi wa Gambia waanza kuhesabu kura za uchaguzi wa rais mjini Banjul, Gambia

8
Maafisa wa uchaguzi wafunga sanduku za kura baada ya upigaji kura kukamilika