Akiwa katika nchi hizo mbili Papa Francis alitoa ujumbe muhimu wa kutaka mapigano na ghasia kukomeshwa mara moja, na kudumishwa kwa amani katika nchi hizo mbili za Afrika ya Kati.
Papa Francis akamilisha ziara yake ya Sudan Kusini na DRC
Papa Francis amekamilisha ziara yake ya siku 6 nchini Sudan Kusini na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, kwa Misa Takatifu kwenye uwanja wa makumbusho wa John Garang, mjini Juba, siku ya Jumapili.

1
Papa Francis yuko ndani ya ndege akirudi Vatican baada ya ziara ya siku sita nchini Sudan Kusini na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo

2
Papa Francis (kati kati) aongoza Misa Takatifu siku ya Jumapili, kwenye uwanja wa makumbusho wa John Garang siku ya mwisho ya ziara yake Sudan Kusini

3
Papa Francis akimuombea Rais Salva kiir wa Sudan Kusini wakati wa sherehe za kumuaga kabla ya kuondoka Juba, Sudan Kuisni

4
Waumini wa Sudan Kusini wakihudhuria Misa inayoongozwa na Papa Francis mjini Juba, Jumapili Feb 5, 2023.