Viongozi wa Afrika watembelea Ukraine kwa juhudi za kumaliza vita vya Rashia na Ukriane
- Abdushakur Aboud
Marais Macky Sall wa Senegal, Hakainde Hichilema wa Zambia Cyril Ramaphosa wa Afrika kusini na Assoumani Azali wa Comoros,watembelea Ukraine kujaribu kutafuta njia za kuwaleta marais Volodomyr Zelensky wa Ukraine na Vladimir Putin wa Rashia kwenye meza ya mazungumzo.

5
Marais Ramaphosa, wa Afrika Kusini, Sall, wa Afrika Kusini, Hichilema, wa Zambia, Assoumani wa Comoros na waziri mkuu wa Misri Madbuly watoka ikulu ya Kyive baada ya kukutana na rais Zelensky wa Ukraine.

6
Rais Zelensky wa Ukraine (kushoto), akihudhuria mkutano na waandishi habari pamoja na viongozi wa nchi za Afrika baada ya mkutano wao mjini Kyiv.

7
Ujumbe wa amani wa viongozi wa nchi za Afrika watoa heshima zao mbele ya kaburi walozikwa watu wengi mjini Bucha.

8
Ujumbe wa viongozi wa Afrika watembelea maonesho ya picha ya watu walouliwa mjini Bucha.