Watu walioshuhudia tukio hilo wanasema vikosi vya usalama vilifyatua mabomu ya machozi na maguruneti ndani ya msikiti, wakati wanaofanya ibada walirusha mawe na vitu vingine kuwalenga askari hao. Shirika la Hilal Ahmar limesema zaidi wa Wapalestina 300 wamejeruhiwa, kati yao 228 walipelekwa hospitali ya karibu. Darzeni ya Wapalestina walijeruhiwa.
Mapambano yazuka tena Jerusalem karibu na msikiti wa al-Aqsa
Mapambano mapya yamezuka Jumatatu kati ya vikosi vya usalama vya Israeli na Wapalestina waliokuwa wanafanya ibada karibu na msikiti wa al-Aqsa mjini Jerusalem Jumatatu.

1
Msikiti mtakatifu wa al-Aqsa

2
Mwanadamanaji wa Kipalestina akiruka vizuizi vinavyo waka moto wakati wa maandamano dhidi ya Israeli kutokana na mvutano uliopo Jerusalem, karibu na makazi ya Wayahudi ya Beit El karibu na Ramallah, katika eneo linalokaliwa kwa mabavu na Israel, Ukingo wa Magharibi, Mei 9, 2021.

3
Vikosi vya usalama vikikabiliana na Wapalestina waliokuwa katika msikitini wakifanya ibada.

4
Vikosi vya usalama vya Israeli vikilinda doria wakati mvutano kati ya Waisraeli na Wapalestina ukiendelea katika maadhimisho ya Mayahudi ya Siku ya Jerusalem, karibu na eneo la Damascus Gate nje kidogo ya eneo la Old City, Jerusalem Mei 10, 2021. REUTERS/Ronen Zvulun