Ibada ya mazishi ya kiserikali yatafanyika katika Kanisa la kitaifa jijini Washington, DC Jumatano, na kufuatiwa na maziko Alhamisi katika eneo la maktaba yake ya urais huko Texas
Mwili wa Rais mstaafu wa Marekani ukiagwa kwenye ukumbi wa Bunge la Marekani
Waombolezaji watoa heshima zao za mwisho mbele ya mwili wa Rais George H.W. Bush ambao umelazwa kwa heshima za kitaifa katika ukumbi wa bunge la Marekani

1
Jeneza la aliekuwa Rais wa Marekani, George W.H Bush, likiwasili katika ukumbi wa Rotunda, Washington, D.C., Desemba. 3, 2018.

2
Rais wa Marekani Donald J. Trump, akiwa na mkewe wake Melania Trump, akipiga saluti kuonyesha heshima kwa mwili wa Rais wa zamani wa Marekani George H.W. Bush katika chumba cha Rotunda kilichoko katika Bunge la Marekani Washington, DC, Desemba 3, 2018

3
Rais Donald Trump na mkewe Melania Trump, wakiwasili kutoa heshima zao za mwisho kwa mwili wa Rais mstaafu George H. W. Bush ukiwa katika ukumbi wa Rotunda, ndani ya Bunge la Marekani, Jumatatu, Dec. 3, 2018 , Washington. (Brendan Smialowski/Pool via AP)

4
Mwanajeshi wa jeshi la majini kutoka manuari ya kivita ya USS George H.W. Bush akiwa anaangalia ndege iliyokuwa imebeba jeneza lenye mwili wa Rais mstaafu George H.W. Bush arrives katika kituo cha jeshi la anga ( Andrews Air Force Base), Maryland, Desemba. 3, 2018.