Wamarekani wanapo omboleza vifo vya wanafunzi 19 wa shule ya msingi ya Robb mjini Uvalde, Texas, wabunge mjini Washington wanaendelea kujadili kwa hamasa suala la kupitisha sheria za kudhibiti umiliki wa bunduki.
Shambulizi katika shule ya msingi Uvalde, Texas
Kijana mwenye umri wa miaka 18 alishambulia kwa bunduki shule ya msingi ya Robb, mjini Uvalde, Texas na kusababisha vifo vya watoto 19 na walimu wawili.

1
Msichana analia, wakati wazazi wawili wakimfariji nje ya kituo cha Willie de Leon Civic Center ambako ushauri nasaha unatolewa kwa familia za waathiriwa mjini Uvalde, Texas, May 24, 2022.

2
Askofu wa San Antonio, Gustavo Garcia-Siller, akiwapa pole na kuwashauri familia nje ya kituo cha Civic Center kufuatia shambulio la bunduki kwenye shule ya Robb Elementary mjini Uvalde, Texas, May 24, 2022.

3
Polisi wapiga doria karibu na shule ya msingi ya Robb Elementary kufuatia shambulio la bunduki, Mei 24, 2022, in Uvalde, Texas.

4
Maafisa wa kikosi maalum cha usalama wakiwa karibu na shule ya msingi ambako shambulizi lilitokea mjini Uvalde, Texas, Mei 24, 2022.