Wizara ya afya ya Uganda ilithibitisha watu 11 wameambukizwa na virusi vya Ebola pamoja na vifo vinne.
Mlipuko wa sasa ambao unahusishwa na aina nadra ya virusi vya Ebola inayopatikana Sudan, ulianzia katika kijiji kidogo cha wilaya ya Mubende mwanzoni mwa mwezi huu wa Septemba, maafisa wamesema.
Vifo vingine saba vinachunguzwa kwa kuhusishwa na mlipuko wa Mubende, wilaya inayopatikana umbali wa kilomita 130 mashariki mwa mji mkuu Kampala.
Kifo cha kwanza kilikuwa cha mwanaume wa miaka 24 ambaye alifariki mapema wiki hii.