Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Mei 16, 2025 Local time: 07:38

Vijana wa Afrika wanufaika na programu ya NBA


Wachezaji wakishindana kuuchukuwa mpira Julai 29, 2019, huko uwanja Diamniadio, Dakar ufunguzi wa michezo wa 17th mpira wa kikapu bila mipaka (BWB) Africa ulioandaliwa na NBA, Shirikisho la Mpira wa kikapu duniani (FIBA) na shirikisho la mpira wa kikapu Senegal.
Wachezaji wakishindana kuuchukuwa mpira Julai 29, 2019, huko uwanja Diamniadio, Dakar ufunguzi wa michezo wa 17th mpira wa kikapu bila mipaka (BWB) Africa ulioandaliwa na NBA, Shirikisho la Mpira wa kikapu duniani (FIBA) na shirikisho la mpira wa kikapu Senegal.

Programu ya Shirikisho la Mpira wa Kikapu Marekani (NBA) bila mipaka imekuwa ikitafuta wachezaji na kuwafundisha wavulana na wasichana barani Afrika kwa miaka 17.

Wasichana walioshiriki katika programu wanasema mafunzo wanayopatiwa na wanawake kutoka bara hilo ambao walikuwa wakichezea timu ya wanawake ya NBA imewahamasisha kuendelea na mchezo huo.

“Uzoefu huu umetusaidia sana kujiongeza kimchezo,” Iris, 16, kutoka Gabon, ameiambia VOA. Hili limenisaidia sana, nimeweza kujifunza vitu vipya na imeweza kunirejeshea mapenzi yangu katika mchezo huu, na matakwa yangu ni kuendelea na mchezo huu na kuja kuwa na jina katika ulimwengu wa mpira wa kikapu.

Iris anasema aliweza kuletwa katika pragramu hiyo na waandaaji ambao waliona timu yake ya nyumbani Gabon ikicheza. Iris aliambiwa azalishe picha ya video akiwa anacheza na baadae alijulishwa kuwa amekubaliwa kujiunga na programu hiyo.

Makocha na washauri hao wanaendelea kuwasaidia wachezaji hao vijana kwa kuwapa mazoezi na kuwachezesha katika mechi mbalimbali, lakini pia wanakuwa ni kiigizo cha kielelezo kwa vijana hao kile wanachoweza kukifikia katika ulimwengu wa mpira wa vikapu.

Moja wa waliofanikiwa na kuwa ni mfano kwao ni Astou Ndiaye, ambaye asili yake ni Senegal. Alikuwa akichezea timu ya Detroit Shock, ambayo ilishinda michuano ya NBA ya wanawake 2003.

“Sisi tumepitia hatua zile zile ambazo wao wanataka kupitia,” Ndiaye ameiambia VOA. “Kuwepo hapa peke yake na kuweza kuzungumza nao, kujibu maswali yao na kuwapa hasa matumaini, uthubutu wanaohitaji kuwa nao ni kama sisi tunaweza, wao pia wanaweza kufikia tulipofikia sisi kuna uwezekano huo kwao.

Ndiaye amekuwa akifundisha vijana wa kike katika programu ya mpira wa vikapu bila ya mipaka kwa miaka mingi, lakini anamatumaini hasa mwaka huu kwa sababu ni mara ya pili tu kwa Senegal kuwa ni mwenyeji wa programu hii yenye historia ya miaka 17.

Kushiriki kwa Ndiaye na hamasa anayoleta katika programu hii ni kichocheo cha kipekee kwa vijana wa kike wengi ambao wanataka kufuata mwenendo wake.

XS
SM
MD
LG