Maafisa wa uchaguzi wanasema kumekuwepo na wapigaji kura wengi walojitokeza katika uchaguzi unaofuatiliwa kwa karibu kupima mfumo wa kidemokrasia wa taifa hilo la Afrika Magharibi.
Wagambia wapiga kura kwenye uchaguzi wa rais
- Abdushakur Aboud
Kwa mara ya kwanza baada ya miaka 27 wananchi wa Gambia washiriki kwenye uchaguzi bila ya hofu kutokana na kutokuwepo na jina la kiongozi wa mabavu Yahya Jammeh.

1
Wafanyakazi wa uchaguzi wa Gambia wahesabu gololi zinazowakilisha kura za kila mtu kwenye uchaguzi wa rais mjini Banjul, Gambia, Dec. 4, 2021.

2
Wafanyakazi wa uchaguzi watumia bao la kuhesabu gololi kuhesabu kura za wapigakura wakati wa uchaguzi wa rais mjini Serrekunda, Gambia,, Dec. 4, 2021.

3
Maafisa wa uchaguzi na wanaojitolewa watayarisha sanduku za kuweka kura mtaani Manjai Kunda

4
Rais Adama Barrow akizungumza kwenye uwanja wa McCarthy baada ya kupiga kura yake Banjul