Rais Biden aliweka shada la maua nje ya jengo ambalo ndege nambari 93 ilianguka huku mvua ikinyesha. Akiwahutubia walohudhuria sherehe hizo, alitaja jinsi wamarekani walivyoungana kujibu mashambulio hayo na kuapa kwamba “kamwe hawatoacha” kuendelea kupigana dhidi ya vitisho vya ugaidi.
Wamarekani waadhimisha miaka 21 tangu mashambulio ya kigaidi ya Septemba 11, 2001
Rais Joe Biden aliongoza ibada kwenye jengo la Pentagon, huku Makamu Rais Kamala Harris akiungana na waombolezi mjini New York na mke wa rais Jill, aliongoza ibada Pennsylvania ili kuwakumbuka watu elfu 3 walofariki kwenye maeneo hayo.

1
Rais Joe Biden akizungumza wakati wa sherehe za Septemba 11, 2022 nje ya jengo la Pentagon.

2
Mke wa rais, Jill Biden akishiriki kwenye sherehe za kuadhimisha miaka 21 tangu mashambuliyo ya kigaidi ya Septemba 11, 2001.

3
Rais Joe Biden akizungumza wakati wa sherehe za Septemba 11, 2022 nje ya jengo la Pentagon.

4
Makamu Rais Kamala Harris na mumewe Doug Emhoff akizungumza na Seneta Chuck Shumer mjini New York wakati wa sherehe za kuadhimisha miaka 21 ya mashambulio ya Septemba 11.