Maoni yake yamekuja siku moja baada ya kutoa wito mpya kwa washirika kutuma mikfumo ya ulinzi wa anga ya Patriot “haraka iwezekanavyo.”
Rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskyy
Ukraine inakabiliwa na mashambulizi ya kila siku ya droni na makombora kutoka Russia, ikiwemo mashambulizi kadhaa katika miji mikubwa na maeneo ya miundombinu ya nishati.
“Sisi bado tunasubiri vifaa tulivyoahidiwa,” Zelenskyy alisema katika hotuba ya kila siku usiku kwa njia ya video Jumapili. “Tunatarajia kiwango kikubwa na chenye upeo mkubwa wa silaha hizo ambazo zinaweza kubadilisha hali ya vita katika eneo la mstari wa mbele kwa maslahi ya Ukraine,” aliongeza kusema.
Zelenskyy alisema alikuwa amemaliza kuzungumza na kiongozi wa walio wachache katika Baraza la Wawakilishi Hakeem Jeffries na kulishukuru Bunge kwa kupitisha mswaada uliokwama wa dola bilioni 61 kwa ajili ya Ukraine.
Hakeem Jeffries
“Katika mazungumzo yangu na Bw. Jeffries, nilisisitiza kuwa mifumo ya Patriot inahitajika, na kwa haraka iwezekanavyo,” aliongeza kusema.
Jeffries alisema katika akaunti ya X kuwa Marekani “itaendelea kusimama na watu wa Ukraine katika ushujaa na ujasiri wenu kupambana na uvamizi wa Russia.”
Majeshi ya Ukraine, ambayo idadi yake imezidiwa na majeshi ya ardhini ya Russia, yanajaribu kurudi nyuma kutoka maeneo ya mashariki mwa Ukraine huku majeshi ya Russia yakisonga mbele upande wa magharibi, Kanali wa Ukraine Jenerali Oleksandr Syrskyi alisema Jumapili.
Baadhi ya taarifa katika repoti hii inatokana na mashirika ya habari ya Reuters, AP na AFP.