Michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika AFCON 2019
AFCON 2019 MISRI : Mpangilio wa Raundi ya 16
Mechi za kwanza Ijumaa zitakuwa baina ya wawakilishi pekee wa Afrika Mashariki, Uganda, dhidi ya Senegal.
AFCON 2019 MISRI : Uganda kuchuana na Senegal raundi ya 16
Mechi za kwanza Ijumaa zitakuwa baina ya wawakilishi pekee wa Afrika Mashariki dhidi ya Senegal katika uwanja wa Cairo International
AFCON 2019 MISRI : Je, utabiri wa mashabiki wa Misri ni kweli?
Misri kuchuana na Afrika Kusini Jumamosi...
AFCON 2019 MISRI Kundi E-F Raundi Ya Pili
Raundi ya pili ya fainali za kombe la mataifa ya Afrika, AFCON, itaanza Ijumaa baada ya kumalizika kwa raundi ya kwanza Jumanne.
Raundi ya 16 ya AFCON yapangika

Raundi ya pili ya fainali za kombe la mataifa ya Afrika, AFCON, itaanza Ijumaa baada ya kumalizika kwa raundi ya kwanza Jumanne na timu 16 kufuzu raundi ya pili zikiongozwa na wenyeji Misri.
Mechi za kwanza Ijumaa zitakuwa baina ya wawakilishi pekee wa Afrika Mashariki, Uganda, dhidi ya Senegal katika uwanja wa Cairo International. Pambano jingine siku hiyo litakuwa baina ya Morocco na Benin katika uwanja wa Al- Salaam mjini Cairo.
Katika raundi hiyo ya pili ambayo itakuwa katika mtindo wa mtoano wenyeji Misri watachuana na Afrika Kusini, DRC itapambana na Madagascar timu ambayo ilikuwa "Cinderella" wa fainali hizi, timu ambayo imeingia katika fainali hizo kwa mara ya kwanza na kushinda kundi lake kwa pointi saba ikiwa ni pamoja na kuifunga timu ngumu ya Nigeria 2-0 katika raundi ya kwanza.
Mechi nyingine za raundi ya pili ni Ghana dhidi ya Tunisia, Mali na Ivory Coast, Algeria dhidi ya Guinea na Nigeria itapambana na Cameroon katika moja ya mechi inayotazamiwa kuwa kali katika raundi ya pili.
Timu za Afrika Mashariki, Tanzania na Burundi zilimaliza mashindano kwa kufungwa mechi zote tatu wakati Kenya ilishinda mechi moja dhidi ya Tanzania na kufungwa na Senegal na Algeria.
Robo fainali za mashindano haya zitaanza Julai 10 na nusu fainali zitakuwa Julai 14 wakati mechi ya fainali ya mwisho itachezwa Julai 19.
Imetayarishwa na mwandishi wetu, Washington, DC
AFCON 2019 MISRI : Kundi D Roundi ya 2
Muhtasari wa mechi ambazo tayari zimechezwa
AFCON 2019 MISRI : Pambano la Burundi, Guinea
Burundi : "Hatujakata tamaa"
AFCON 2019 MISRI : Wakenya washangilia ushindi wa timu yao ya taifa
Wanawake wa Kenya wakiwa na bashasha baada ya timu yao ya taifa kuifunga timu ya Tanzania magoli matatu kwa mbili.
AFCON 2019 MISRI : Kenya yaifunga Tanzania
Mshabiki wa Kenya atabiri mechi ya Tanzania na Kenya
AFCON 2019 MISRI : Hali ilivyokuwa Jijini Cairo
Wamisri wakisheherekea ushindi baada ya kuifunga DRC 2-0.
AFCON 2019 MISRI : Muhtasari wa mechi zilizochezwa
Mechi za timu mbalimbali ambazo zimecheza
AFCON 2019 MISRI : Wapenzi wa Soka kutoka nchi mbalimbali za Afrika

Mke wa Rais mstaafu wa Tanzania Salma Kikwete akiwa miongoni mwa waliosafiri kushuhudia AFCON na kuhamasisha timu ya Tanzania.
Misri ni nchi yenye utamaduni wake yakiwemo mavazi na vinywaji. Lakini katika michuano ya kombe la AFCON watu wa kutoka mataifa mbalimbali pia wanashiriki katika kuhamasisha wachezaji kutoka nchi zao.
AFCON 2019 MISRI : Mchekeshaji Na Msanii Wa Tanzania Atoa Nasaha Zake
Mchekeshaji na msanii Pierre Liquid akizungumza na mwandishi wa VOA Sunday Shomari nchini Misri, Jumanne
AFCON 2019 MISRI : Uchambuzi : Tanzania vs Senegal
Mchambuzi Abdullah Matitu wa Tanzania akieleza mapungufu yaliyojitokeza katika mechi ya Tanzania na Senegal.