Waandamanaji hao waliharibu baadhi ya sehemu ya jengo hilo ikiwemo madirisha na Milango.
Wafuasi wa Rais Trump wafanya uharibifu jengo la Bunge la Marekani
Wafuasi wa Rais wa Marekani Donald Trump wavunja sheria za usalama na kuvamia ndani ya Bunge la Marekani wakati likiwa linajadili kuthibitishwa kwa kura za wajumbe za matokeo ya uchaguzi wa rais, January 6, 2021.

1
Wafuasi wa Rais Donald Trump wakipambana na maafisa wa polisi na vikosi vya usalama walipokuwa wakijaribu kuingia katika Bunge la Marekani ambalo lilikuwa limetanda moshi wa mabomu ya kutoa machozi mjini Washington, DC on Januari 6, 2021.

3
Wafuasi wa Rais wa Marekani Donald Trump wakiandamana ndani ya eneo la Bunge Marekani linalojulikana kama Rotunda Januari 6, 2021, in Washington, DC.

4
Wafuasi wa Rais wa Marekani Donald Trump wakusanyika kupinga kuthibitishwa kwa matokeo ya uchaguzi ya kura za wajumbe waliopiga kwa Rais mteule Joe Biden, mjini Washington, DC Januari 5, 2021. (Photo by SAUL LOEB / AFP)

5
Wafuasi wa Rais Donald Trump wakikabiliana na maafisa wa polisi katika Bunge la Marekani, Washington, 6 Januari 2021.