Wanajeshi wa Israel wamepambana vikali na wapiganaji wa Hamas Jumapili karibu na hospitali kubwa kabisa ya Gaz, Al Shifa ambako maelfu ya watu wamekwama.
Baraza la Usalama la Umoja wa mataifa limepinga Jumatatu usiku mswada wa azimio ulowasilishwa na Rashia unaolaani ghasia zinazoendelea Mashariki ya Kati.
Rais Joe Biden wa Marekani amesisitiza wakati wa mkutano na waandishi habari akiwa Hanoi, Vietnam kwamba hana nia ya kuidhibiti China, wakati nchi hizi mbili zinazidi kutofautiana juu ya masuala ya biashara, usalama na haki za binadam.
Watu 20 wamefariki nchini Uchina na zaidi ya watu 350 000 wamehamishwa kufuatia mafuriko yaliyotokana na moja wapo ya vimbunga vibaya kutokea kusini Mashariki ya Asia.
Wajumbe wa kamati ya Mamlaka ya Ushirikiano wa Serikali za Afrika Mashariki na Pembe ya Afrika, IGAD, ya kutafuta suluhisho kwa mzozo wa Sudan, wamekutana mjini Addis Ababa Jumatatu kujadili namna ya kusitisha mapigano na uhasama na kurudisha utulivu nchini humo.
Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron ametoa wito kwa wazazi kuwazuia watoto wao kushiriki katika ghasia zinazoendelea kwa usiku wa tatu nchini mwake, huku akisema baadhi ya vijana wanaonekana wakiiga michezo ya video kusababisha ghasia.
Karibu mahujaji milioni mbili wamewasili mlima Arafat, kuanzia alfajiri Jumanne, ikiwa ndio kilele cha ibada ya Hajj, ikiwa ni idadi ndogo kuliko vile serikali ya Saudi Arabia ilivyotarajia baada ya kuoindolewa masharti yaliyowekwa tangu janga la COVID.
Karibu mahujaji milioni 2 wamewasili kwenye Mlima Arafat, kuanzia alfajiri Jumanne, ikiwa ni kilele cha ibada ya Haji na mahala ambako ina aminika Mtume Mohamed SWA, alitoa hotuba yake ya mwisho.
Rais Vladimir Putin amepinga mpango wa amani ambao viongozi wa nchi za Afrika walikua na matumaini utaweza kumaliza vita na Ukraine, walipokutana nae mjini St. Petersburg, siku ya Jumamosi.
Marais Macky Sall wa Senegal, Hakainde Hichilema wa Zambia Cyril Ramaphosa wa Afrika kusini na Assoumani Azali wa Comoros,watembelea Ukraine kujaribu kutafuta njia za kuwaleta marais Volodomyr Zelensky wa Ukraine na Vladimir Putin wa Rashia kwenye meza ya mazungumzo.
Mke wa rais wa Marekani Jill Biden amewasili Nairobi Ijumaa tarehe 24, Februari akiwa katika ziara ya mataifa mawili ya Afrika, Namibia na Kenya akifuatana na mjuku wake Naomi
Juhudi za uwokozi kufuatia tetemeko kubwa la adhri nchini Uturuki na Syria zimeingia siku ya tano Ijuma, kukiwa na matumaini madogo kabisa kuweza kupata watu zaidi hai, ingawa kumekuwepo na watu walookolewa Ijuma kutoka baadhi ya miji.
Papa Francis aliwasili Kinshasa Jumanne Januari 31, na kutoa wito kwa Jumuia ya Kimataifa kutojihusisha ndani ya masuala ya Afrika, na kuwaachia waafrika watanzuwe matatizo yao wenyewe.
Viongozi wa Afrika Mashariki na Kati wamezungumzia juhudi za kupatikana amani mashariki ya Jamhuri ya Kongo, walipokutana mjini Washington, kando ya Mkutano wa viongozi kati ya Marekani na Afrika Mapema mwezi Disemba.
Dunia yashuhudia matukio ya kihistoria mwaka 2022 kuanzia mabadiliko ya hali ya hewa, vita vya Ukraine, ughali wa maisha hadi nja na uhamiaji.
Mamilioni ya wamarekani wamelazimika kufutilia mbali mipango ya kusherehekea siku kuu ya Krismasi kutokana na baridi kali kuwahi kushuhudiwa baada ya miongo kadhaa, huku maafisa wa serikali katika majimbo mengi wakiwashauri watu kubaki majumbani.
Akizungumza wakati wa mkutano wa viongozi wa Afrika na Marekani kiongozi wa Uganda amesema walijadili ghasia zinazoendelea katika kanda ya Maziwa Makuu na wanaamini wataweza kutanzua mzozo uliyopo.
Majengo mengi katika mji mkuu wa Qatar Doha yaliwashwa taa usiku wa Jumamosi kuonesha picha ya bingwa wa kandanda wa Brazil Pele ikimtakia afueni ya haraka.
Pandisha zaidi